Alhamisi, 31 Desemba 2015


Kwa nini Mlima Kilimanjaro uko Tanzania na si Kenya?

Mlima Kilimanjaro
MPAKA wa Tanzania na Kenya ni wa ajabu na ni wa kushangaza pia. Tofauti na mipaka mingine ya nchi yetu upande wa Mashariki, Kusini na Magharibi, Mpaka huo wa Kaskazini umechorwa kwa mstari ulionyooka kana kwamba ulichorwa kwa msaada wa rula kuanzia Bahari ya Hindi, kuelekea Kaskazini hadi Ziwa Victoria.
Kwa jinsi ulivyoanza, mstari huo ulipaswa kwenda moja kwa moja Kaskazini Magharibi, na kuutupa nje Kaskazini Mlima Kilimanjaro uwe ndani ya Kenya, badala ya kuwa Tanzania ilivyo sasa. Lakini, pengine kwa sababu maalumu, mchoraji aliupaisha juu Kaskazini zaidi makusudi ulipokaribia Mlima huo, kisha ukapinda tena kuelekea Kaskazini Magharibi kwa unyoofu ule ule, kuhakikisha kwamba Mlima wote unakuwa ndani ya Tanzania badala ya Kenya; na kuendelea hadi Ziwa Victoria kwa kunyooka vivyo hivyo.
Kwa nini, nani kitu gani hasa kilimfanya mchoraji wa Mpaka huo kupindisha mstari huo kufanya Mlima Kilimanjaro uwe nchini Tanzania, badala ya kuwa nchini Kenya?
Mnyukano wa Wajerumani na Waingereza
Kuna dhana inayovuma kwamba, Malkia wa Uingereza, Victoria; alimpa zawadi mjukuu wake, mtawala (Emperor) wa Ujerumani, Wilhelm Mlima huo mwaka 1886, kwa sababu mjukuu huyo alipenda vitu vikubwa.  Dhana hii si sahihi kwa sababu mwaka huo, Wilhelm hakuwa mtawala wa Ujerumani, bali Babu yake. Lakini jibu sahihi linatokana na Mataifa ya Ulaya kugombea Afrika (Scramble for Africa), mnyukano uliokamilishwa na Mkutano wa Berlin kwa mataifa hayo kukaa meza moja kuchora mipaka (partition) kuigawana Afrika.
Mnyukano huo ulishika kasi ya kutisha katikati ya miaka ya 1880, Uingereza ikiongoza na kufuatiwa na Ufaransa; huku Ujerumani nayo ikijikakamua kutoachwa nyuma katika kuwania makoloni.
Desemba 4, 1884, Sultani Mangungu wa Usagara (Msovelo) alisainishwa Mkataba wa “Urafiki” na Jasusi la Kijerumani, Karl Peters, bila kujua kwamba alikuwa anauza nchi yake kwa Wajerumani na kuitwa “Deutch –Ostafrika”, yaani “Afrika Mashariki ya Wadachi/Wajerumani” na kuimilikisha Kampuni ya Kijerumani iliyojulikana kama “German East African Company” (GEAC).
Februari 1885, Karl Peters aliomba ulinzi wa Kampuni yake kwa Kiongozi wa Ujerumani (Emperor), Bismarck, na kupewa barua ya kukubaliwa (Imperial Letter of Protection) kupata ulinzi wa maeneo (nchi) yote yaliyochukuliwa na GEAC upande wa Bara Magharibi mwa Dar es Salaam, na maeneo ya Uzigua, Ukaguru na Usambara ambako machifu 10 wa maeneo hayo walisaini Mikataba “kumuuzia” nchi zao bila kujua.
Ilichotaka GEAC ni kupata njia huru na Bandari kwenye Bahari ya Hindi, na hivyo kuzua mgongano na Sultani wa Zanzibar aliyeshikilia Pwani yote, kutoka Somalia upande wa Kaskazini hadi Rasi Delgado (Msumbiji) upande wa Kusini; na pia Bara yote iliyokuwa njia ya misafara ya Watumwa hadi Maziwa Makuu.
Na pale Sultani Sayyid Barghash alipoonesha jeuri ya kutokubali matakwa ya Wajerumani, Manowari ya kivita ya Kijerumani ilitia nanga Bandari ya Zanzibar na kuelekeza mitutu ya mizinga kwenye Kasri lake, naye akasalimu amri hima.  Wakati huo Zanzibar ilikuwa chini ya usimamizi na ulinzi wa Uingereza (British Protectorate) kwa Mkataba maalumu.
Kuona hivyo, Februari 26, 1886, Waziri Mkuu wa Uingereza wa wakati huo, Lord Salisbury, aliingilia kati akiamini kwamba, haki za Zanzibar juu ya eneo lote la Pwani zilikuwa wazi, ingawa hakuwa na uhakika juu ya ukomo wake Kaskazini (Somalia?), lakini alifikiri umbali wa maili 60 ulimtosha Sultani. Alijua kuwa, himaya ya Sultani ilijumuisha pia Wilaya za Kilimanjaro na Uchagani; alisema:  “Eneo lote la Wilaya ya Kilimanjaro kamwe haliwezi kuwa chini ya ulinzi wa bendera nyingine (mbali ya Sultani au Uingereza) bila kuathiri maslahi ya Uingereza”.
Wababe wote walikuwa na mikataba
Ni kwamba, Waingereza, Wajerumani na Sultani mwenyewe, wote walikuwa na mikataba waliyoingia na Machifu wa Kichaga kutambua himaya za wababe hao, kama tu alivyofanya Chifu Mangungu.  Mmoja wa Mikataba ya Machifu hao 25 na Sultani, uliotiwa sahihi Mei 30, 1885, ulisomeka hivi:
“Sisi Masultani (machifu) wa Uchagani na Kilimanjaro, tunaapa mbele ya Jenerali Mathews na Askari wake na Wafuasi, kwamba, tunatambua kuwa (sisi) ni watawaliwa wa Mtukufu Sultani wa Zanzibar, na hivyo tunapeperusha bendera yake juu ya minara nchini mwetu kuthibitisha utii wetu kwake, na kuwa,tunamtambua kama mtawala/mfalme wetu”.
Mkataba huo wa pamoja ulitiwa sahihi (dolegumba) na Machifu Mandara wa Moshi, Kitungeti wa Kirua; Marealle wa Muranju (Marangu), Mitanuvi wa Mamba, Fumba wa Kilema, pamoja na Machifu wa Machame, Rombo, Taveta na wengineo.
Mandara alitia sahihi Mkataba mwingine kama huo na Mjerumani wa GEAC, Dakta Karl Juhlke, Juni 11, 1885, kumpa mamlaka yote na haki ya kuchukua na kutumia ardhi, kutoza kodi na ushuru, pamoja na kuanzisha utawala wake na Mahakama; kuvuna Mlima Kilimanjaro, Mito, Maziwa na Misitu yote.
Kubadilishana na haki hizo, Mandara alihakikishiwa ulinzi, yeye na mali zake, pamoja na elimu kwa watoto wake. Akitoa shukrani kwa Dakta Juhlke na GEAC, Mandara alisema: “Nawapenda sana Wajerumani kuliko mataifa mengine yote; zaidi kuliko Waingereza hasa, nani kwako pekee (wewe Juhlke) nitatoa nchi yangu”.
Hatimaye, baada ya kubaini kwamba alikuwa njia panda, Mandara alilalama akisema:  “Sultani wa Zanzibar anataka nchi yangu; Wajerumani, vivyo hivyo nao wanataka nchi yangu; ninyi (Waingereza) mnataka nchi yangu pia! Aitakaye nchi yangu atakiona cha mtema kuni”. Hakutaja aina ya “cha mtema kuni” hicho.
Tume ya maridhiano yaundwa
Kutokana na kindumbwendumbwe hicho, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani ziliunda Tume ya Maridhiano kubainisha mipaka kwa kuzingatia maeneo ya ushawishi wa nchi hizo kuepuka ugomvi, lakini Sultani hakushirikishwa.
Mijadala ndani ya Tume ilikuwa mikali, kila mshiriki akivutia upande wake.  Mwakilishi wa Ujerumani alitaka kutumia Bandari ya Dar es Salaam iliyokuwa chini ya himaya ya Sultani, bila kutozwa kodi.
Pili, alitaka Sultani apunguziwe eneo la himaya upande wa Pwani ili abakie na urefu wa maili kumi tu; pia kwamba, madai ya Sultani huyo juu ya eneo la Kilimanjaro yasitambuliwe.
Tatu, Ujerumani ilitaka kampuni zote za Uingereza zilizokuwa eneo la Kilimanjaro ziondoke na zikubali kulipwa fidia ili Mjerumani ashike eneo lote hilo.
Kwa GEAC, Kilimanjaro lilikuwa jambo la kufa na kupona, na ilikuwa tayari kwa lolote kutoiachia; kama ambavyo tu Zanzibar ilivyokuwa muhimu kisiasa na kiuchumi kwa “Emperor”  Bismarck wa Ujerumani kiasi kwamba, nchi hiyo ilikuwa na Ubalozi mdogo Visiwani humo tangu mwaka 1884 kuonesha umuhimu huo.
Uingereza na Ufaransa zilionesha kuunga mkono madai ya Sultani dhidi ya matakwa ya Ujerumani. Kwa kupewa ujasiri na msimamo wa nchi hizo, wakati mazungumzo yakiendelea, Sultani alituma kikosi chenye Askari 200, kikiongozwa na Jemedari wa Kiingereza, Jenerali Mathews, kwenda eneo la Kilimanjaro kusimika bendera nyekundu ya himaya yake. Wakati wakirejea, walipambana na Kikosi cha Wajerumani karibu na Taveta, kilichofika huko kwa madhumuni hayo hayo; mapigano yakazuka, lakini yakakoma sawia kwa maelekezo ya Tume ya Maridhiano iliyokuwa ikiendelea na kikao.
Wakati huo huo, Mwakilishi wa Uingereza, Sir Percy Anderson, alikuja na wazo la kati katika kutatua ugomvi wa Ujerumani na Uingereza kuhusu eneo la Kilimanjaro, la kuligawa sehemu mbili kuwapa Wajerumani nusu ya upande wa Kusini, na nusu ya Kaskazini wapewe Waingereza.
Pendekezo hilo lilipingwa vikali na Wajerumani kwa madai kwamba isingekuwa rahisi kuligawa hivyo eneo hilo lenye mlima na vilima, hivyo wakasisitiza wapewe eneo lote peke yao. Sir Percy alitupa hoja yake kutafuta suluhu mbadala.
Mombasa yatibua mambo
Ikazuka hoja kuhusu nani adhibiti Mombasa (bandari) ambayo ilikuwa chini ya himaya ya Sultani, lakini yenye kuwaniwa vikali na Uingereza na Ujerumani pia.  Wajerumani walitaka wawe na Bandari Pwani ya eneo hilo na (iwe) njia fupi kuufikia Mlima Kilimanjaro kwa urahisi, na kwamba, Mombasa ulikidhi madhumuni haya kwavile ulikuwa katikati ya maeneo ambayo Ujerumani ilikuwa ikiwania upande wa Kaskazini na Kusini.
Waingereza hawakuwa tayari kupoteza Mombasa, kufa na kupona; kama ambavyo tu Wajerumani hawakuwa tayari kupoteza Kilimanjaro. Jemadari wa Kiingereza, Luteni Kanali Kitchner, tayari alikuwa ameshinikiza kukamatwa kwa Mombasa ili kiwe Kituo cha Manowari zakivita za Uingereza na ghala kuu la silaha katika bahari ya Hindi.
Nao wafanyabiashara na Wamissionari wa Kiingereza,walioweka vituo na Makao Mombasa, hawakutaka Serikali yao kuachia bandari hiyo pamoja na njia za biashara “kuangukia kwenye udhibiti wa Taifa shindani” kwani, kwa maoni ya Sir Percy, Uingereza ingekosabarabara ya uhakika hadi Ziwa Victoria “unakoanzia Mto Nile,na hivyo kuwa vigumu kuifikia Sudani ya Chini”. Kufikia hapo, mazungumzo yaligota na hali ya kutoaminiana kutawala.
Mpaka mpya:  Taveta hadi Victoria
Ili kukidhi matarajio yake, Sir Percy aliwasilisha pendekezo la pili, la Mpaka unaoanzia Kusini mwa Mombasa kuelekea Taveta, kisha unapanda juu sehemu ya Kaskazini mwa Kilimanjaro (kuuingiza ndani mlima huo), na kuambaa hadi Mashariki mwa kingo za Ziwa Victoria, kama unavyoonekana leo.
Kwa pendekezo hili la pili, Ujerumani iliamua kuachia Mombasa na kukubali kutia sahihi Mkataba wa makubaliano kwa kuridhika kwamba maeneo Kusini ya mpaka huo yaliyobakia mikononi mwake, yalikidhi kiu yake ya makoloni kufanya ijishughulishe kwa muda mrefu uliofuata.
Mkataba huo, uliofikiwa Novemba 1, 1886, ulielezea mpaka huo ifuatavyo:  “Mstari wa Mpaka unaanzia kwenye mdomo wa Mto Wanga au Umbe,unakwenda moja kwa moja hadi Ziwa Jipe; unapita upande wa Mashariki mwa Ziwa na kupinda tena upande wa Kaskazini kabla ya kuvuka mto Rumi; kisha unachana katikati ya nchi ya Taveita (Taveta) na Uchagga; unaambaa chini ya kitako cha Mlima Kilimanjaro kwenda juu kuelekea Kaskazini; kisha unanyooka tena moja kwa moja na kutua upande wa Mashariki wa kingo za Ziwa Victoria Nyanza”.
Huo ndio ufafanuzi kwa maneno ya kidiplomasia, wa Mpaka kati ya Tanganyika (wakati huo ikiitwa Deutch – Ostafrika) na Kenya uliopo hadi leo. Chini ya makubaliano hayo, Ujerumani, kupitia Kampuni ya GEAC, ilijipatia Mlima Kilimanjaro na kupoteza Mombasa; na Waingereza kujipatia Mombasa na kupoteza Mlima Kilimanjaro.
Januari 1, 1891, maeneo yote ya GEAC yaliingizwa kwenye himaya ya Serikali ya Ujerumani kuruhusu uvamizi na uingiliaji kijeshi wa maeneo hayo,yakiwa tayari milki halali ya nchi hiyo.
Kutoka Deutch – Ostafrika hadi Tanganyika
Sultani wa Zanzibar kwa upande wake, alibakiziwa kipande cha urefu wa maili 10 tu za Pwani, ambacho miaka miwili baadaye, mwaka 1888, alikikodisha kwa Wajerumani kisha akapokonywa kwa nguvu mwaka huo huo na Wajerumani hao.
Wakati wa utawala wa Kijerumani, nchi yetu iliitwa “Deutch – Ostafrika”; na baada ya vita ya kwanza ya Dunia mwaka 1918, ambapo Waingereza walichukua nchi kutoka kwa Wajerumani, iliitwa “Tanganyika Territory”, jina lililopendekezwa na Mwingereza, Sir Cosmo Parkinson, kabla ya kuitwa kwa kifupi “Tanganyika” baada ya vita ya tatu ya Dunia, mwaka 1945.
Mipaka rasmi ya iliyokuwa “Deutch –Ostafrika” (Tanganyika), iliridhiwa Machi 22, 1921, kufuatia Mkataba wa amani uliofikiwa kati ya Uingereza na Ujerumani ambapo, kabla ya hapo, eneo lote la sasa la Kigoma na Biharamulo, lilikuwa chini ya Wabelgiji.
Kwa madhumuni ya mada hiini kwamba, Mlima Kilimanjaro upo Tanzania kwa sababu mji wa Mombasa uko Kenya, ikiwa ni matokeo ya minyukano ya mataifa mawili ya Kikoloni, Ujerumani na Uingereza.  Na hilo hatuna nguvu nalo kwa kuwa historia sharti itawale.
Hapa tunapata fundisho pia; kwamba, Watawala wetu wa leo, wanaoingia Mikataba kimbumbumbu na kizembe na kina “Karl Peters” wa zama hizi,katika madini na ardhi, kama walivyofanya Chifu Mangungu wa Musovelo [Usagara]  na Chifu Mandara wa Moshi; waelewe kwamba, wanatuweka rehani kwa wawekezaji hao chini ya ukoloni mpya, sisi na hatima yetu.  Kwa sababu hii, tusishangae kuona siku mojatukivamiwa na wawekezaji hao, wakitumia majeshi ya nchi mama, pale tutakapoamka kutoka usingizini kudai ardhi rasilimali tunazoporwa.  Huku ni kukaribisha historia kujirudia, kwa kilio na kusaga me

Jumatatu, 28 Desemba 2015

Unaijua Vyema Historia ya Mzee Mandela??: Hebu pita hapa upate japo kwa ufupi



Rais wa kwanza wa Afrika Kusini,Mzee Nelson Mandela

Imeandikwa na Abubakari jumbe wa   Africatradition.blogspot.com.                  


Kila ifikapo18 Julai ni kumbukumbu ya kuzaliwa Mzee Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini ya Kidemokrasia (18.07.1918). Kadri ya kumbukumbu zangu huyu ndiye mtu pekee ambaye Umoja wa Mataifa umemtengea siku katika mwaka mahususi kwa heshima yake. Hivi leo anatimiza miaka 93 toka azaliwe; ni mmoja kati ya viongozi wachache wa Afrika ambao wameishi kwa muda mrefu.

Nelson Mandela ni mtu anayepewa heshima kubwa duniani kote kwa wanaomfahamu na hata wasiomfahamu. Watu wengi hasa nje ya Afrika hususani katika jamii zinazopenda kusoma vitabu wanamfahamu kupitia kitabu chake cha "Long Walk to Freedom". Hiki ni kitabu kinachoelezea historia ya maisha yake kwa kina kabisa. Sehemu kubwa ya kitabu hicho ameandika yeye mwenyewe na tena akiwa gerezani. 

 Hili ni moja ya mambo ya kujifunza toka kwa mzee huyu-maktaba kubwa duniani kote. Tujipange tuandike historia zetu sahihi ili kuiachia jamii na dunia kwa ujumla utajiri wa mawazo kama alivyofanya mzee Mandela. Wengine tulimfahamu mzee Madiba toka enzi za utoto; tukiwa shule ya msingi tuliimba nyimbo za kutaka Mandela aachiwe huru na serikali ya makaburu. Utawala wa makabulu ulitawala Afrika Kusini kwa mabavu na kwa misingi ya kibaguzi ya rangi za binadamu; ni udhalimu wa aina yake kwa ustawi wa wanadamu.

Kwanini mzee huyu ni maarufu?

Kwa hakika sifahamu yote juu ya mzee huyu anayependwa mno si tu kwake huko Afrika Kusini bali pia duniani kote kwa ujumla, hilo ladhihirika kwa Umoja wa Mataifa (UM) kumtengea siku maalum ya kumuenzi.
Mandela, alifungwa katika magereza tofauti kwa jumla ya miaka 27; umri wa kijana aliyekomaa. Mwanasiasa huyo, ambaye alikuwa pia Mwanasheria, mwanamichezo na mpigania haki za watu, alifungwa na serikali ya Makaburu kwa walichokiita uhaini. 

Nelson Mandela moja ya vijana walionzisha madai ya uhuru kwa njia ya mapigano alikuwa na imani kuu juu ya haki sawa kwa watu wote. Aliamini na anaamini kuwa binadamu wote ni sawa katika misingi ya ubinadamu- kwa haki na mahitaji yetu. Ni kwa imani na msukumo huo wa kudai uhuru na haki za watu wote wa Afrika Kusini ndo alikuwa tayari kudai haki hizo hata kama ingemlazimu kuyatoa maisha yake; funzo kubwa hilo.

Kwa hakika imani juu ya haki sawa kwa watu wote ni funzo na changamoto kubwa kwa viongozi wote duniani. Nini imani yako wewe kiongozi juu ya haki sawa kwa wananchi unaowaongoza? Ni dhahiri kuwa unatambua kuwa wananchi wako wote wanahitaji chakula cha kutosha, makazi, huduma muhimu za kijamii; afya, elimu, na kadhalika (nk). 

Lakini tunacho kishuhudia hii leo ni ubinafsi mkubwa wa viongo na hata wananchi wengine wenye nafasi bila kujali mahitaji ya wengine wenye haja ya vile vitu tu vya msingi. Wasomi wengi katika nchi zetu zinazoendelea tunahangaika na mahitaji ya ziada ila hali kuna wenzetu wengi tu wasio na mahitaji yao ya lazima. Tukitaka kutambulika vyema hapa duniani ni lazima tujifunze kwa mzee Mandela kujisahamu kwa ajili ya wengine.

Baada ya kuachiwa huru mwaka 1990 alirejea kwenye harakati za kudai haki za Waafrika Kusini walio wengi. Mwaka 1991 alichaguliwa rais wa "African National Congress" ANC Mandela alichaguliwa kuwa rais wa kwanza wa Afrika Kusini ya kidemokrasia mwaka 1994. Alitumikia muhula mmoja tu wa miaka mitano na mwaka 1999 kuacha mamlaka ya dola kuu kabisa kiuchumi barani Afrika. Utaona kuwa Mzee Madiba alifanya kinyume kabisa na viongozi wengi wa barani mwetu.

Suala kuu ambalo dunia imejifunza toka kwa mzee huyu wa miaka 93 sasa ni moyo wa msamaha. Kumbe hata kwa binadamu msamaha unawezekana. Msamaha huu umeongozwa na busara kuu bila shaka na neema tele za Mwenyezi Mungu. 

 Rais Nelson Mandela angeweza kabisa kulipa kisasi cha Waafrika Kusini weusi wengi waliopoteza maisha kwenye harakati za kujikomboa, lakini hakufanya hivyo, alisamehe na badala yake aliwaunganisha wananchi wote wa Afrika Kusini mpya, ingawa kuna vidonda vingi na makovu watakayoishi nayo daima, na kuanza kuijenga nchi yao kwa manufaa yao wote. 

Hii ni changamoto kuu kwa wanadamu wote - nadhani ni sababu hii hasa ndo imeulazimu Umoja wa Mataifa kuanzisha siku mahususi kumuenzi mpigania haki za binadamu Nelson Mandela Madiba. Kwa hakika Madiba ni mjenga dunia!!

Ukoloni ni Nini??

Ramani ya ukoloni duniani mwishoni mwa Vita Kuu ya Pili ya Dunia mwaka 1945.
Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za kiuchumikiutamadunina kijamii. Maeneo haya yanaweza kuitwa koloni au eneo lindwa.
Ukoloni unaitwa hasa kipindi tangu karne ya 15 ambako Ureno na Hispaniazilianza kuenea Afrika na Amerika ya Kusini na kudumu hadi baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Lakini kulikuwa na vipindi vya ukoloni pia zamani katika historia kama vile ukoloni wa Roma ya Kale, ukoloni wa Waarabu na vingine. Ukoloni kwa maana hii inaweza kuwa tofauti na kuundwa kwa koloni katika vipindi mbalimbali vya historia ambako maeneo bila wakazi au penye wakazi wachache sana yaliingiliwa na watu kutoka sehemu nyingine.

Nchi za Afrika ziliwekwa chini ya ukoloni wa nchi za Ulaya mara baada yaMkutano wa Berlin ulioitishwa nachansella wa Ujerumani Bismarckmwaka 1884-1885.
Nchi zilizojenga ukoloni huu wa Afrika zilikuwa UingerezaUfaransaUreno,UjerumaniUhispaniaItalia na Ubelgiji.
Ukoloni mamboleo ni aina ya nchi au kundi la nchi fulani kutawala nchi nyingine kinyemela kwa kuweka vikwazo na masharti yatakayowafanya watawaliwa waendelee kuwa na uchumi tegemezi ili wawatajirishe zaidi hao wanaowatawala kinyemela

Jumapili, 27 Desemba 2015

VITA VYA MAJI MAJI



Vita ya Maji Maji ulikuwa upingaji mkali wa Waafrika katika Tanganyika Kusini dhidi yautawala wa kikoloni katika koloni laUjerumani ndani ya Afrika Mashariki.
Vita hivyo vilishirikisha baadhi ya makabila ya kusini mwa Tanzania ya leo dhidi ya utawala wa Kijerumani katika kukabiliana na sera ya Kijerumani iliyoundwa kwa nguvu kuwalazimisha watu wa Tanganyika kulima zao lapamba.
Vita hivyo vilidumu kuanzia mwaka1905 hadi 1907.

  WAJUWE  WAMASAI NA HISTORY YAO KIUJUMLA

Page issues
Wamasai
Maasai women and children.jpg
Wamasai, Kenya, 2005.
Wamasai ni kabila wazawawa Afrika la watu wahamaji katika wanaopatikana Kenya na kaskazini Tanzania. Kwa sababu ya mila tofauti zao na mavazi na kuishi karibu na mbuga nyingi za Afrika Mashariki, wao ni miongoni mwa wengi ya makabila yanayojulikana Afrika. [1] Wao wanazungumza Maa[1]mojawapo ya familia ya lugha ya Nilo-Saharainayohusiana na Dinka naNuer, na pia wameelimika katika lugha rasmi za Kenya na Tanzania:Kiswahili na Kiingereza. Idadi ya Wamasai inakadiriwa kuwa 377.089 kutoka Sensa ya 1989 [2]au kama lugha ya wasemaji 453.000 nchini Kenya mwaka 1994 [3] na 430.000 katika Tanzania mwaka 1993 [3] kwa jumla inakadiriwa kuwa "inakaribia 900.000" [1]Makadirio hayo ya Wamasai katika nchi zote mbili huenda ikawa ni vigumu kuyathibitisha kwa sababu ya umbali wa maeneo ya vijiji vyao vingi, na asili yao ya uhamaji.

Ingawa serikali ya Tanzania na Kenyaimeweka mipango kuwahimiza Wamaasai kuachana na asili yao ya jadi ya uhamaji, bado wameendelea na desturi hiyo. [4] Hivi majuzi, Oxfamimedai kwamba mtindo wa maisha ya Wamasai lazima ikubaliwe ili kuzingatia mabadiliko ya hali ya hewa kwa sababu hawana uwezo wa kulima katika majangwa. [5]

Jumamosi, 26 Desemba 2015

  FAHAMU ZAIDI KUHUSU Lefto

HISTORIA YA MJI WA KILWA PAMOJA NA MAJENGO YA KALE



Mwanzo wa Kilwa umekadiriwa ulikuwa mnamo 800 BK. Kuna kumbukumbu ya kimdomo inayosema: Watu wa kwanza waliojenga Kilwa Kisiwani ndio Watakata, halafu watu wa Jasi wa kabila la Waranga. Badaaye akaja Mrimba na watu wake. Halafu akaja Sultan Ali bin Selimani Mshirazi yaani Mwajemi. Akaja na jahazi zake akaleta bidhaa na watoto wake. Mtoto mmoja aliitwa Fatima binti Sultan Ali. Hatujui majina ya watoto wengine. Walikuja na Musa bin Amrani Albedu. (kutoka BBC: The Story of Africa - The Swahili).





Kuanzia karne ya 11 Kilwa ilikuwa kituo muhimu ya biashara. Kuanzia karne ya 13 na 14 BK Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka Dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka Bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.





Katika karne ya 14 -kati ya 1330 na 1340 BK- mji ulitembelewa na msafiri Mwarabu Ibn Battuta aliyeacha taarifa ya kwanza ya kimaandishi kuhusu mji. ajengo makubwa yalijengwa ikiwa magofu yao yamesimama hadi leo kama vile msikiti kuu, nyumba ya kifalme ya Husuni Kubwa na mengi mengine.

Kuja kwa Wareno katika Karne ya 16 ilivuruga biashara ya Waswahili. Kilwa ikarudi nyuma. Katika karne za 18. na 19. ikapata upya nguvu ya kiuchumi kutokana na biashara ya watumwa. Mwisho wa biashara hii ulimaliza utajiri wa Kilwa.
 

 Sehemu ya jengo ambalo lilikuwa na ukumbi mkubwa wa kunadi bidhaa zikiwemo watumwa,pembe za ndovu,simbi,mbao na vyombo vya kufinyangwa kutoka bara la Arabu na Ghuba ya uajemi,kisha kuingiza kwenye ngarawa tayari kwa kusafirisha (Maelezo haya ni kwa ajili ya picha ya hapo juu). 

Kilwa Kisiwani ni jina la kijiji kikubwa kwenye Kisiwa cha Kilwa karibu na mji wa Kilwa Masoko katika Mkoa wa Lindi, Tanzania. Ndipo mahali pa mji wa Kilwa ya kihistoria iliyokuwa mji mkubwa kabisa kati ya miji ya Waswahili katika pwani la Afrika ya Mashariki wakati wa karne za 12-15 BK. Kwa hivyo, Kilwa ilikuwa mji mkuu Afrika mashariki kabla ya wazungu hawajafika kwenye bahari kuu la Hindi.

Kwa mujibu wa tariki ya Kilwa ambayo ni miongoni mwa matini ya kizamani sana yanayotoa historia fupi kuhusu sehemu hii ya Tanzania, Kilwa ni mji ulioanzishwa na kusimamishwa na wahamiaji kutoka Shiraz, huko Uajemi kwa siku za leo. Ni dhahiri kwamba matini haya ambayo jina la mtunzi wake limepotea ni aina ya masimulizi ya kusisimua akili ya msomaji kwa kuwa na hadithi ya kibuni.

Kwa hivyo, ingawa yana maudhui ya kuvutia sana kutokana na ushuhudio wake muhimu sana, tariki hizi hazisomeki kama insha ya kisayansi ambayo itakuwa imeandikwa kufuatana na nadharia tete yenye uthabiti. Mintarafu asili ya wahamiaji wa kwanza ambao walifika Kilwa, hatuna uhakika kwamba walikuwa wanatoka Uajemi, kama inavyodaiwa na tariki hii. Hapo tuwe makini sana.

 Kwa mujibu ya tariki hizi, inasemekana kwamba Sultani mmoja aliyeitwa Hassan bin Ali kutoka Shirazi ndiye aliyehama kule kwao wakati wa kuibuka aina ya mgogoro kati ya watu wake. Sultani huyo akaamua kuondoka na watoto wake sita. Kuondoka kwao huko kwenye bandari ya Siraf, walisafiri kwa jahazi saba kuelekea Afrika mashariki. Hapo inaaminika kuwa kila wakipita kwenye bandari ya kanda ya pwani, mmojawapo alivunja safari yake huku akiaamua kuweka misingi ya mji wake.



Ndiyo asili ya miji saba ambayo tunayo mpaka leo kwenye kanda ya pwani ya afrika mashariki : Mandakha, Shaughu, Yanba, Mombasa, Pemba, Kilwa na Hanzuân. Sultani mwenyewe alikuwa wa mwisho katika kusalia katika msafara huu, naye akakaa kisiwa cha Hanzuani ambacho kipo Ungazija. Mikasa hii na tukio hilo limejitokeza katika miaka kuanzia 957 mpaka 985 baada ya K. Inaaminika kwamba Kilwa wakati ule kilikuwa kisiwa kilichomilikiwa na wenyeji waitwao wamuli.

Kwa kuwa walikuwa hawana nguvu nyingi, walikubali kukiuza kisiwa chao kwa kukubali kupewa vipande vya ntandio. Hapo ndipo Ali bin Hussein alipochukua kisiwa hiki kwa ajili ya kukaa ikiwa ni pamoja na kujenga majumba ya kujitetea dhidi ya watu wa bara na miji mingine ya pwani.

 Kati ya mwaka 957 hadi 1131, Kilwa uliwahi kupambana na mji jirani uliokuwa unaitwa, kwa enzi zile, Shagh. Ghasia zile zikakolea, zikawa zikageukia zikawa vita kwa ajili ya kutawala himaya kubwa. Kilwa ukawa na sifa za fahari katika pande zote za Afrika mashariki kutokana na nguvu zake na mali yake ambayo ilikuwa inatoka bara la Afrika, pahala panapoitwa Sofala. Dhahabu ya Sofala, ambayo ilikuwa ni baadhi ya madini iliyopatikana kwa wingi wakati ule, ilikwenda kuchukuliwa na kuletwa Kilwa kwa njia ya kutembea kwa miguu. Misafara hii ilikuwa changamoto kubwa sana katika kutajirisha himaya ya Kilwa.




Hapo si kiwanja ila ni ukumbi amabo mnada ulikuwa ukifanyika,au sherehe zao watawala hao wa kiarabu walikuwa wakifanyia humo,kwa mbele kuna maji ni bahari ambapo kuna ngazi za kuteremshia bidhaa kuingiza kwenye ngarawa zao.fika ukajionee ni utalii nafuu zana wa kuona kisiwa cha kihistoria Tanzania. (Maelezo haya ni picha ya juu).
Hapo yupo mwandishi mwingine katika lugha ya kiarabu, Al-Mutahar bin Tahir al Makdisi, ambaye vile vile anatoa ushahidi mzuri wa kwamba nchi ya zenj – ambayo ni sehemu hii ya kanda ya pwani kwa enzi hizo – ilichangia sana katika usafirishaji wa dhahabu kutoka Kilwa kwenda Uarabuni kuanzia karne hii ya 10.

Kwa kifupi, wataalamu wa historia wamekubali kusema kwamba kilele cha Kilwa katika kujifaharisha kilianza karne 12 ikadumu hadi karne 15. Kilwa ikawa muhimu zaidi kuliko Mombasa. Biashara yake ilikuwa dhahabu kutoka dola la Mwene Mtapa (Zimbabwe), pembe za ndovu, chuma, nazi pamoja na kununua bidhaa kutoka bara Hindi na Uchina. Sarafu ya dhahabu kutoka Kilwa imepatikana huko Zimbabwe Kuu.

Baharia maarufu ambaye pia alikuwa ni mwana historia hodari sana, Ibn Battuta, anathibitisha vilevile kwamba dhahabu ilikuwa inapatikana pia katika eneo lililoitwa Yufi, nchini mwa Limi (nchi ya kiajabu ambayo wataalamu wengine wanakisia ni pengine Nigeria). Zama zile zilikuwa za kudhabiti utawala wa Kilwa ambao ulipanua mpaka Mafia, Zanzibar na Pemba. Sultani Suleiman bin al-Hassan (1170-1189) aliwahi kukarabati majengo makubwa ya Kilwa kisiwani. Anajulikana sana kwa ujenzi aliouanzisha chini ya utawala wake ambao unaitwa Husuni mdogo. 

Enzi hii bado ilikuwepo chini ya nasaba (dynastie) ya Shirazi mpaka mwaka 1277, ambapo ni kipindi cha awamu nyingine iliyojitokezea katika nasaba ya Mahdaliya ambayo ilitoka Hadramau, Yemen. Karne 14 na mwanzoni mwa karne 15 zilikuwa nyenzi za fahari kubwa sana kwa sababu ya kufaidi na kujiimarisha kipindi kile cha nyuma ambacho Sultani Al Hassan bin Suleiman II (1331-1332) alipopata nafasi ya kuongeza nafasi ya kuswalisha swalat al ijumaa ikiwa ni pamoja na kujenga kasri inayojulikana kwa jina la Husuni Kubwa. 

                                                       Hii Ndiyo Ramani ya Kilwa
 Hicho ni kiberenge kilitumiwa na mmoja wa mwanaakolojia ambaye akikuwa akichimba ili aone masalia ya vyombo vilivyo kuwa zikitumika wakati huo na washirazi kisiwani hao wakati huo.aliyeshika kiberenge ni Bw.samweli mtembeza wattalii.