Utamaduni
Neno la Kilatini lenye maana ya utamaduni ni Cultura ambalo lina usuliwake katika neno colere, linalomaanisha "kulima, kustawisha".[1]
Neno hili linafafanuliwa namna nyingi. Kwa mfano, mnamo mwaka 1952,Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohnwalikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno hilo katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions.[2]
Hata hivyo, neno "utamaduni" linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:
- Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu
- Mkusanyo wa maarifa ya binadamu,itikadi na tabia ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kwa njia ya ishara
- Jumla ya mitazamo, kaida, malengona maadili yanayotambulisha asasi,shirika au kikundi fulani
Dhana hii ilipoibuka kwanza katikakarne ya 18 na 19 barani Ulaya, ilimaanisha mchakato wa kulima au kuboresha kilimo au kilimo cha mboga. Katika karne ya 19 dhana hii ilimaanisha kuboreshwa kwa mja kupitia elimu na hali kadhalika ilimaanisha kutekelezwa kwa maazimio ya kitaifa au maadili.
Katikati ya karne ya 19, wanasayansiwengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.
Katika karne ya 20, "utamaduni" ulijitokeza kama dhana ya msingi katikasomo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote ya binadamu ambayo hayakufungamana namaumbile.
Dhana ya utamaduni katikaAnthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili: (1) Uwezo wa binadamu wa kuainisha na kuwasilisha tajiriba za kibinadamu kiishara na kutenda mambo kiubunifu; na (2) Namna mbalimbali ambazo watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni huainisha na kuwasilisha tajiriba zao za maisha na kutenda mambo kiubunifu. Kufuatia vita vya pili vya dunia, dhana hii ilipata umaarufu ingawa kwa fafanuzi tofautitofauti katika taaluma kama vilesosholojia, mafunzo ya utamaduni,saikolojia ya mipangilio na mafunzo yausimamizi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni