Ijumaa, 22 Januari 2016

Picha ya karne ya 19 inayoonyesha wakazi wa Australia wakipinga kuwasili kwa Kapteni James Cook mwaka 1770
Uvumbuzi wa utamaduni unaamanisha uvumbuzi wowote mpya na unaopatikana kuwa wa manufaa kwa kikundi cha watu na unaelezewa katika tabia zao lakini haupo kama kitu kinachoonekana. Watu wako katika ulimwengu unaoharakisha mabadiliko ya utamaduni kiwakati,wakisukumwa na kupanuka kwa biashara kimataifa,vyombo vya habari,na kuongezeka kwa idadi ya watu miongoni mwa mambo mengine.
Tamaduni zinaathiriwa na nguvu zinazoleta mabadiliko na zile zinazopinga mabadiliko. Nguvu hizi zina uhusiano na miundo ya kijamii na matukio halisi na zinajihusisha katika kuendeleza mawazo na matendo ya kitamaduni ndani ya miundo ya sasa ambayo nayo inabadilika[186]. (Tazamaumuundo.)
Mizozo ya kijamii na maendeleo ya kiteknolojia yanaweza kusababisha mabadiliko katika jamii kwa kubadili mikikimikiki ya kijamii kwa kukuza ruwaza mpya za utamaduni kwa kuwezesha tukio zalishi. Hii mihamisho ya kijamii huweza kuandamana na mihamisho ya kiitkadi na aina nyingine za mabadiliko ya kitamaduni. Kwa mfano muungano wa kifeministi wa Kimarekani ulihusisha matendo mapya yaliyosababisha uhamisho katika mahusiano ya kijinsia,kubadilisha jinsia na miundo ya kiuchumi. Hali ya kimazingira inaweza kuchangia. Mabadiliko huhusisha kufuata nguli wa kienyeji katika filamu. Kwa mfano,misitu ya kitropika ilirejea tena mwishoni mwa enzi ya theluji.mimea iliyofaa kwa kufugwa ilikuwepo,ikasababisha kuvumbuliwa kwa kilimo,ambacho kilisababisha uvumbuzi wa kitamaduni na mihamisho ya mikikimikiki ya kijamii[187].
Picha kamili ya mwanamke wa Turkman,akisimama kwenye zulia katika mlango wa yurt,akiwa amevalia nguo za kitamaduni pamoja na virembesho
Tamaduni huathirika kutoka nje kupitia kwa mwingiliano baina ya jamii,ambazo pia zinaweza kutoa—au kuzuia---mihamisho ya kijamii na mabadiliko katika matendo ya kitamaduni. Vita au ushindani juu ya rasilimali unaweza kuathiri maendeleo ya kiteknolojia na mikikimikiki ya kijamii. Kuongezea,mawazo ya kitamaduni yanaweza kuhama kutoka jamii moja hadi nyingine kupitia kwa kuenea na kwa mabadiliko ya uigaji wa utamaduni Fulani. Katika kuenea hali ya kitu(siyo lazima maana yake) hutoka utamaduni mmoja hadi mwingine. Kwa mfano,hamburgers ambazo ni za kawaida Marekani,zilionekana kuwa ngeni zilipoanzishwa Uchina. "Kuenea kunakoacha athari” (kubadilishana mawazo) hurejelea elementi za utamaduni mmoja kusababisha kuwepo kwa uvumbuzi au kusambazwa.kwa mwingine. "Ukopaji wa moja kwa moja” kwa upande mwingine hurejelea kuenea kwa kiteknolojia au kuenea kunakoonekana kutoka utamaduni mmoja hadi mwingine. Nadharia ya kuenea kwa uvumbuzi huwasilisha ruwaza ya utafiti ya kwa nini na lini watu na tamaduni huasilisha mawazo mapya,matendo na bidhaa.
Kuiga utamaduni fulani kuna maana tofauti lakini katika muktadha huu hurejelea kubadilishwa kwa tabia Fulani za utamaduni na utamaduni mwingine.Haya yamefanyika kwa makabila fulani ya Amerika na kwa makundi asilia ya watu kote ulimwenguni enzi za ukoloni. Michakato ya karibu kwa kiwango cha binadamu inahusisha usilimisho (binadamu kuasilisha utamaduni fulani) na kuwa na tamaduni nyingi.

                     Utamaduni

Michoro mwambani huko Gobustan,Azerbaijan10000 KK ikionyesha utamaduni uliostawi.
Jumba la Kiajemi Hasht-Behesht.
Utamaduni ni jinsi binadamuanavyokabili maisha katika mazingirayake.
Neno la Kilatini lenye maana ya utamaduni ni Cultura ambalo lina usuliwake katika neno colere, linalomaanisha "kulima, kustawisha".[1]
Neno hili linafafanuliwa namna nyingi. Kwa mfano, mnamo mwaka 1952,Alfred Kroeber na Clyde Kluckhohnwalikusanya orodha ya vijelezi 164 vya neno hilo katika kazi yao: Culture:a Critical Review of Concepts and Definitions.[2]
Hata hivyo, neno "utamaduni" linatumika kimsingi katika njia tatu zifuatazo:
  • Maonjo ya hali ya juu katika sanaa, vilevile hujulikana kama utamaduni wa juu
  • Mkusanyo wa maarifa ya binadamu,itikadi na tabia ambao hutegemea sana uwezo wa kuwasilisha mawazo na mafunzo ya kijamii kwa njia ya ishara
  • Jumla ya mitazamo, kaida, malengona maadili yanayotambulisha asasi,shirika au kikundi fulani
Dhana hii ilipoibuka kwanza katikakarne ya 18 na 19 barani Ulaya, ilimaanisha mchakato wa kulima au kuboresha kilimo au kilimo cha mboga. Katika karne ya 19 dhana hii ilimaanisha kuboreshwa kwa mja kupitia elimu na hali kadhalika ilimaanisha kutekelezwa kwa maazimio ya kitaifa au maadili.
Katikati ya karne ya 19, wanasayansiwengine walitumia dhana ya utamaduni kurejelea uwezo wa kiubia wa binadamu.
Katika karne ya 20, "utamaduni" ulijitokeza kama dhana ya msingi katikasomo la Anthropolojia. "Utamaduni" ulihusisha mambo yote ya binadamu ambayo hayakufungamana namaumbile.
Dhana ya utamaduni katikaAnthropolojia ya Kimarekani ilikuwa na maana mbili: (1) Uwezo wa binadamu wa kuainisha na kuwasilisha tajiriba za kibinadamu kiishara na kutenda mambo kiubunifu; na (2) Namna mbalimbali ambazo watu wanaoishi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni huainisha na kuwasilisha tajiriba zao za maisha na kutenda mambo kiubunifu. Kufuatia vita vya pili vya dunia, dhana hii ilipata umaarufu ingawa kwa fafanuzi tofautitofauti katika taaluma kama vilesosholojia, mafunzo ya utamaduni,saikolojia ya mipangilio na mafunzo yausimamizi.

Jumatatu, 4 Januari 2016

KINJEKITILE NGWALE NA HISTORIA YENYE UTATA!

Kulikuwa na mateso na kulimishwa kwa nguvu.
Leo katika kupekua kwangu mtandaoni, nimekutana na historia mbili tofauti zinazomzungumzia Kinjekitile. Kilichonivutia hadi kuamua kuwashirkikisha wasomaji wa kibaraza hiki ili tutafakari kwa pamoja ni kutokana na kupingana kwa historia hizo.

Wakati historia moja ikihoji kuwa Kinjekitile alikuwa shujaa au mshirikina? ambayo iliandikwa na mwandishi Aloyce Menda katika gazeti la Tanzania Daima la Ijumaa, Septemba 21,2006, nyingine ilikuwa ikidai kuwa historia yake imepotoshwa, ambayo nayo iliandikwa na mwandishi Evaristy Masuha katika gazeti hilo hilo la Tanzania Daima la Alhamisi, Agosti 21, 2008.

Kwa historia hizo mbili kunaonekana kuwa na walakini na ni vyema historia hii ikawekwa sawa kwa manufaa ya vizazi vijavyo, la sivyo tutajikuta tukiwa tumepoteza kumbukumbu hii muhimu kwa vizazi vyetu.

Naomba tuwekane sawa katika swala hili, Je ni yupi yuko sahihi kati ya waandishi hawa wawili?

***************************************